Picture Gallery Send us feedback

NEWS

DIAMOND ASHINDA TUZO TATU KWA MPIGO

Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.

Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.

KILIMANJARO PREMIUM LAGER, BONGE LA KIBURUDISHO KWA WATANZANIA

 
Habari zaidi