






Aloyce Joseph (kushoto) na Daniel Ngowi wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager illi kusherekea miaka 50 ya Uhuru.

Kundi la wanariadha wanaoshiriki katika Mbio za Bendera ya Taifa za Kili likiwasili katika Mji wa Korogwe Mkoani Tanga juzi. Jumla ya Wanariadha 30 wanaikimbiza bendera hiyo wakitokea Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kupitia kampeni ya "Jivunie Utanzania" inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambapo wataungano na wenzao kutoka mikoa mingine ili kuipandisha katika Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru

Wanariadha wa timu ya Mwanza (kulia) na Timu ya Dodoma wanaoshiriki katika mbio za Bendera ya Taifa za Kili kutoka Mjini Mwanza na Dodoma walipokutana katika Mji wa Karatu mkoani Manyara wakielekea mjini Moshi ambapo jumla ya wanariadha 60 walikimbiza bendera za rangi ya njano na Nyeusi kupitia Kampeni ya Jivunie utanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya KIlimanjaro Premium Lager.(Picha na Mpigapicha wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki akikabidhi bendera kwa wanariadha wanaoshiriki katika mbio za bendera ya Taifa ambazo ni sehemu ya Kampeni ya Kili Jivunie Utanzania inayoenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Uhuru, wakati akiwaaga Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi (katikati) akianzisha mbio za Bendera ya Taifa Za Kili Mjini Dodoma jana ambapo aliwaaga wanariadha 30 wanaokimbiza bendera hiyo kuelekea Moshi kupitia Kampeni ya Jivunie uTanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya KIlimanjaro Premium Lager.
Maadhimisho ya miaka kumi ya Mbio za Kilimanjaro yanayotarajiwa kufanyika Februari 26, 2012 kwa ufadhili wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, yamezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema wadhamini wameamua kuongeza zawadi za washindi katika mbio hizo kwa asilimia 100.

Viwango vya zawadi za mbio za Km 42.195 kwa washindi wa mbio za wanawake na wanaume. Mshindi wa kwanza 6,000,000/=; Mshindi wa pili 3,000,000/=; Mshindi wa tatu 1,700,000/=
2012 Kili Marathon itafanyika Jumapili 26/02/2012, Muccobs Stadium Moshi. Click below to download 2012 Kili Marathon Entry Form
2012 Kili Marathon Entry Form English Version
2012 Kili Marathon Entry Form Swahili Version

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi fungu la udhamini kwa msanii wa muziki wa Bongo Flava Juma Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa aliyechaguliwa kushindania tuzo za Channel O za Video bora ya Muziki kutoka Afrika Mashariki
7th November 2011

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Kilimanjaro Premium Lager imezindua rasmi mbio za Bendera ya Taifa ambazo ni sehemu ya Kampeni ya 'Jivunie uTanzania' inayokwenda sambamba na maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya TBL jijini Dar es Salaam na kuwaleta pamoja baadhi ya wanariadha watakaoshiriki katika mbio hizo pamoja na viongozi wa chama cha Riadha Tanzania. Mbio hizi zinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Kushiriki katika promosheni ya maswali yaliopo kwenye chupa ya Kili, andika jina kamili na Jibu kisha tuma kwenda No 15723 nasi tutakupigia simu na utakuwa na nafasi ya KUSHINDA zawadi kemkem. Sikiliza Clouds FM kwa maelezo zaidi
Bonyesha hapa upate maswali na majibu
Mwisho wa promosheni ni 9 December 2011

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Steve Kilindo akisalimiana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Mwitongo Butiama wakati baadhi ya viongozi wa Kampuni hiyo walipomtembelea Jumanne wiki hii kama sehemu ya Kampeni ya Jivunie uTanzania.

Wanenguaji wa kundi la muziki wa dansi la Extra Bongo, wakicheza show wakati kundi hilo lililopotoa burudani kali katika tamasha la Kili jivunie Utanzania lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Mbeya katika viwanja vya CCM Ilomba.

Kaimu Kamnada wa Polisi Mkoa wa Mbea, Anaclet Marindisa akizindua rasmi maandamano ya amani ambayo ni sehemu ya tamasha la Kili Jivunie Utanzania liliyofanyika Mkoani Mbeya Jumamosi
TANZANIA Breweries Limited through its Kilimanjaro Premium Lager brand organised an event dubbed Kilimanjaro Fun Festival to launch Kilimanjaro 'Jivunie uTanzania' Campaign.
A statement issued in Dar es Salaam on Tuesday July 12th and signed by the Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager, George Kavishe, said the event was in line with this year's celebration of Tanzania's 50 years of Independence.