HABARI/NEWS

TBL Kili Marathon Sh 20 milioni

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetangaza udhamini wa Shilingi milioni 20 kwa mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika February 28, 2010 Mkoani Kilimanjaro.

Akitangaza udhamini huo jana, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Bw. George Kavishe alisema udhamini huo ni sehemu ya jitihada za kampuni yake kusaidia maendeleo ya michezo nchini na kwamba zawadi za msimu ujao zitaongezeka mara dufu.

Bw. George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
"Tumeongeza fedha hadi kufikia milioni 20, kiwango ambacho ni kikubwa kutolewa kama zawadi katika mashindano yote ya riadha hapa nchini.

"Natumaini ongezeko la zawadi litawapa moyo wanariadha wetu na kufanya vizuri zaidi katiak mashindano hayo na kuvunja rekodi zilizopo ili waweze kupata nafasi ya kushiriki mbio kubwa zaidi za kimataifa,"alisema Shelukindo.

Alisema mchezo wa riadha ndio mchezo pekee ulioiletea Tanzania sifa kubwa kwenye anga za kimataifa na akaongeza kuwa ushirikino kati ya kampuni yake na chama cha riadha utasaidia kuboresha viwango vya riadha nchini.

TBL imekuwa ikidhamini mashindano hayo tangu mwaka 2003 na mwaka jana yalishirikisha washiriki 35,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Naye mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali Idd Kipingu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliishukuru TBL kwa kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza riadha nchini.