





The oldest national level annual competition which was established in the mid 1940’s under the name of Sunlight Cup.
The current name - Taifa Cup was introduced in 1971 after the first major amendments in the national FA Constitution. The participating teams are regional combine teams. Mbeya are the current title holders after their triumph against Mwanza in the 2011 edition.
t
Mbeya Captain Ivo Mapunda lifts the 2011 Kili Taifa Cup
Trophy after victory over Mbeya.
TIMU ya soka ya mkoa wa Mbeya, 'Mapinduzi Stars' imengia fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kuichapa Kagera 'Lweru Eagles' kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mchezo huo uliopigwa kwa dakika, 120 baada ya matokeo kuwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida za mchezo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kwa matokeo hayo, Kagera itakutana na Mwanza 'Mwanza Heroes' katika mechi ya fainali itakayochezwa Jumapili. Mwanza iliingia fainali baada ya kuichapa Ilala mabao 2-1.
Mshambuliaji wa Mbeya, Gaudence Mwaikimba alikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Kagera kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 24 baada ya kipa wa Kagera, Msafiri Davo kumchezea rafu mshambuliaji wa Mbeya, Said Mtupa.
Katika mechi hiyo, timu zote mbili zilikuwa zikicheza soka ya nguvu na ushindani kila wakati huku kila timu ikihitaji nafasi ya kufunga bao, ambapo katika dakika ya 60, Themi Felix aliisawazishia Kagera bao na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi kumalizika dakika 90 za mchezo.
Felix alifunga bao hilo baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Mbeya kiasi cha kumfanya golikipa wa Mbeya, Ivo Mapunda kushindwa kuokoa mpira huo.
Baada ya kuongezwa kwa dakika 30 timu zote mbili zilifanya mabadiliko huku Mbeya ikinufaika na mabadiliko hayo yaliyosababisha mashambulizi ya nguvu katika goli la Kagera kiasi cha kuwafanya mabeki wa Kagera kujifunga katika dakika 93 ya mchezo.
Kocha wa Mbeya, Jacob Kilyanga akilizungumzia pambano hilo alisema mechi ilikuwa ngumu, lakini wakashinda hivyo anajiaandaa kubeba ubingwa atakapoitoa Mwanza.
Naye kocha wa Kagera, Juma Mwambusi alisema yaliyopita si ndwele bali anaganga yajayo na lazima aibuke na ushindi katika nafasi ya tatu baada ya kukosa nafasi ya kwanza na nafasi ya pili.
Wakati huo huo, baada ya Mwaikimba kung'ara katika kupachika mabao katika mashindano hayo, pamoja na mshambuliaji wa Mwanza, Jerry Tegete kupachika mabao pia washambuliaji hao wamekuwa gumzo mjini Arusha.
Washambuliaji hao wawili wanagombea kiatu cha dhahabu hivi sasa, na mashabiki wa soka mjini Arusha wameanza kugawana timu ya kushangilia kufutia kandanda safi iliyoonyeshwa na wachezaji hao tangu mashindano yalipoanza katika mji huu wa utalii.
Vinara hao wa ufungaji wanatarajiwa kuwa na vita kali ya ufungaji katika mechi ya fainali itakayochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Timu ya Mkoa wa Kagera baada ya kufungwa na Mbeya sasa itacheza mechi ya kuwania mshindi wa tatu dhidi ya Ilala.
Michuano hiyo ya Kili Taifa Cup imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager.